Friday, August 28, 2009

UKIMWI


Kwanza UKIMWI ni upungufu wa kinga mwilini,na ugonjwa huu unasababiswa na virusi vinavyoitwa VVU.Ugonjawa huu umekuwa ni moja ya magonjwa makubwa sana duniani kwani mpaka sasa bado haujapata kinga,wanasayansi wanakesha usiku na mchana lakini bado hawajaupatia kinga.Ugonjwa huu ni hatari sana,na zifuatazo na baadhi ya dalili zake,homa za mara kwa mara,kuharisha,kupungua uzito,nywele kupoteza afya,na nyinginezo.Madhara yake ni makubwa hasa hasa kwa watoto kwani watoto wenghi huachwa yatima na huu ndio unakuwa mwanzo wa umaskini ukifuatiwa na wtoto walioachwa yatima kujiingiza katika vitendo visivyofaa na mwishoe na wao kufa na ugonjwa ule ule ambao na UKIMWI.Kwa hali hii ugonjwa huu unaonekana kama mzunguko kati yetu sisi binadamu,mwisho ningependa kuwashauri hasa hasa vijana wenzangu kuwa makini na maisha yao kwani UKIMWI unaua.

No comments:

Post a Comment